// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA YATINGA MAKUNDI KIKUBWA, YAICHAPA CBE 6-0 ZENJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA YATINGA MAKUNDI KIKUBWA, YAICHAPA CBE 6-0 ZENJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 21, 2024

    YANGA YATINGA MAKUNDI KIKUBWA, YAICHAPA CBE 6-0 ZENJI


    MABINGWA wa Tanzania, Yanga wamefuzu Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika inayochezwa kwa mtindo wa makundi baada ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya timu ya Benki ya Biashara Ethiopia, CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora, mabao ya Yanga yamefungwa na Mzambia, Clatous Chama dakika ya 35, mzawa Clement Mzize dakika ya 46, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 74 na 90’+3, mzawa Mudathir Yahya dakika ya 88 na Mkenya, Duke Abuya dakika ya 90.
    Kwa matokeo hayo, Yanga inafuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla wa 7-0 kufuatia kuichapa CBE SA 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita bao la Mzimbabwe, Prince Dube dakika ya 45’+1 Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YATINGA MAKUNDI KIKUBWA, YAICHAPA CBE 6-0 ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top