BAO la dakika ya tano la kiungo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Maxi Mpia Nzengeli limeipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi tisa katika mchezo wa tatu, wakati KMC inabaki na pointi zake tano za mechi sita sasa.
0 comments:
Post a Comment