TIMU ya Tanzania leo imechapwa na Afrika Kusini kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa pili michuano ya Kuendeleza Vipaji, Talent Development Scheme (TDS U17) uliofanyika Uwanja wa Bingerville Uwanja wa Bingervile mjini Bingervile nchini Ivory Coast.
Ikumbukwe mechi ya kwanza Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu Aggrey Morris ilitoa sare ya kufungana mabao 2-2 na Zambia hapo hapo Uwanja wa Bingerville juzi na Jumamosi itakamilisha mechi zake za michuano hiyo kwa kucheza na wenyeji, Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment