TIMU ya Tanzania leo imetoa sare ya kufungana mabao 2-2 na Zambia Uwanja wa Bingerville nchini Ivory Coast kumenyana na Zamba katika michuano ya Kuendeleza Vipaji Afrika, Talent Development Scheme (TDS U17) Uwanja wa Bingervile mjini Bingervile nchini Ivory Coast
Katika michuano hiyo iliyoanza jana mjini humo na itaendelea hadi Septemba 7, mabao ya Tanzania yamefungwa na Idrisa Kassim na Mohamed Shila.
Tanzania watarudi uwanjani hapo keshokutwa kumenyana na Afrika Kusini, kabla ya kukamilisha mechi zao kwa kucheza na wenyeji, Ivory Coast Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment