• HABARI MPYA

        Sunday, September 08, 2024

        TANZANIA YACHAPWA KWA MATUTA NA IVORY COAST MICHUANO YA TDS


        TIMU ya Tanzania jana ilikamilisha mechi zake za michuano ya Kuendeleza Vipaji, Talent Development Scheme (TDS U17) kwa kufungwa kwa penalti 5-4 na wenyeji, Ivory Coast kufuatia sare ya 2-2 Uwanja wa Bingerville mjini Bingervile nchini Ivory Coast.
        Mechi mbili za mwanzo za michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) - Tanzania ilitoa sare ya kufungana mabao 2-2 na Zambia, kabla ya kufungwa kwa penalti 4-3 na Afrika Kusini kufuatia sare ya 1-1 mechi zote zikipigwa Uwanja wa Bingerville Uwanja wa Bingervile. 

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: TANZANIA YACHAPWA KWA MATUTA NA IVORY COAST MICHUANO YA TDS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry