KIKOSI cha timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars kimewasili salama nchini Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) dhidi ya Guinea Jumanne kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro.
Taifa Stars ilianza kwa kusuasua kampeni za kuwania tiketi ya AFCON ya mwakani baada ya kulazimishwa sare ya bila mabao na Ethiopia Jumatano Uwanja w Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wao, Guinea baada ya kichapo cha 1-0 jana kutoka kwa wenyeji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa – wanaanza safari ya kuelekea Yamoussoukro.
DRC nao wanasafiri kuja Dar es Salaam kumenyana na Ethiopia Jumatatu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dr es Salaam.
Jumla ya nchi 52 zinashiriki hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya AFCON 2025, mchuano ulioanza jana na utaendelea hadi Novemba 19 mwaka huu – na washindi wawili wa makundi yote 12 watatengeneza idadi ya timu 24 wakiwemo wenyeji Morocco katika Fainali za AFCON ya mwakani.
0 comments:
Post a Comment