WENYEJI, Tabora United wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Matokeo hayo yanaifanya Tabora United ifikishe pointi saba katika mchezo wa nne, wakati Tanzania Prisons inafikisha pointi tatu katika mchezo wa tatu.
0 comments:
Post a Comment