// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TABORA UNITED YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KWA BAO LA PENALTI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TABORA UNITED YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KWA BAO LA PENALTI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, September 11, 2024

    TABORA UNITED YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KWA BAO LA PENALTI


    BAO la mkwaju wa penalti la kiungo Mnigeria, Shedrack Asiegbu dakika ya 32 limetosha kuipa Tabora United ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
    Shedrack Asiegbu (25) aliyesajiliwa kutoka Rivers United FC ya kwao, Umuabali, Abia - alifunga bao hilo baada ya kiungo Mburkinabe, Yacouba Songné kuangushwa kwenye boksi.
    Ushindi huo wa pili katika michezo mitatu ya mwanzo wa msimu unaifanya Tabora United ya kocha Mkenya, Francis Kimanzi ifikishe pointi sita baada ya kufungwa 3-0 na Simba Jijini Dar es Salaam kabla ya kushinda 2-1 dhidi ya Namungo huko Ruangwa.
    Kwa upande wao, Kagera Sugar ya kocha Mganda, Paul Nkata inapoteza mechi ya tatu mfululizo baada ya zile mbili za nyumbani walizofungwa 1-0 na Singida Black Stars na 2-0 mbele ya Yanga.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TABORA UNITED YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KWA BAO LA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top