VIONGOZI, benchi la ufundi na wachezaji wa Simba wamepata nafasi ya kukutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi leo mchana baada ya kuwasili visiwani Zanzibar katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu na kumkabidhi zawadi ya jezi Rais Dkt. Mwinyi pamoja na mke wake, mama Mariam Mwinyi.
Akizungumzia katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu, Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza Simba kwa namna inavyoiwakilisha vyema nchi kimataifa kwani jambo hilo linasaidia kukuza utalii kupitia michezo.
Rais Dkt. pia Mwinyi amesema serikali yake imejipanga kuendelea kuboresha na kujenga viwanja vya michezo ambavyo vitakuwa na vigezo vya kutumika kwenye michuano ya AFCON 2027 na CHAN 2025 hivyo kuikaribisha Simba muda wowote kuja kuchezea hapa michezo ya mashindano ya ndani na kimataifa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo lakini pia ametumia nafasi hiyo kuwasilisha ombi la Simba kupata eneo ambalo tutajenga kituo cha kukuzia vipaji vya mpira wa miguu (academy).
Simba imewasili Zanzibar mchana wa leo tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuanza Saa 2:14 usiku, ukiw mchezo wa kwanza kihistoria wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania kufanyika visiwani humo, lakini mwendelezo wa mashindano ya Bara kupelekwa huko kuanzia ASFC na Ngao ya Jamii.
0 comments:
Post a Comment