• HABARI MPYA

        Wednesday, September 11, 2024

        SIMBA SC LEO WANALALA UTURUKI MAPEMA KESHO WANAUNGANISHA LIBYA


        KIKOSI cha Simba SC kimewasili Istanbul, nchini Uturuki mchana wa leo ambako kitalala kabla ya kuunganisha safari mapema kesho kwenda Tripoli nchini Libya kwa ajili ya mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika Ijumaa.
        Simba itakuwa mgeni wa Al Ahli Septemba 13 Uwanja wa Juni 11 Jijini Tripoli katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
        Wachezaji waliopo kwenye timu za taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 wataungana na wenzao Jijini Istanbul usiku wa leo kwa safari ya Tripoli kesho.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: SIMBA SC LEO WANALALA UTURUKI MAPEMA KESHO WANAUNGANISHA LIBYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry