// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); REFA WA ZAMANI MAARUFU NCHINI, OMAR ABDULKADIR AFARIKI DUNIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE REFA WA ZAMANI MAARUFU NCHINI, OMAR ABDULKADIR AFARIKI DUNIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 13, 2024

    REFA WA ZAMANI MAARUFU NCHINI, OMAR ABDULKADIR AFARIKI DUNIA


    MWENYEKITI wa Chama cha Marefa wa Soka Tanzania (FRAT), Omar Abdulkadir Isasc usiku wa kuamkia kwenye hospital ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
    Abdukadir ambaye ni refa wa zamani wa Kimataifa nchini aliyefanya kazi kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kisukari kwa muda. 
    Msiba upo nyumbani kwake, Mtoni kwa Aziz Ally na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
    Moja kati ya mechi za kukumbukwa alichezesha Abdulkadir ni Fainali ya Kombe la Tusker baina ya watani wa jadi, Machi 31, mwaka 2002 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambayo Simba iliichapa Yanga 4-1.
    Mabao ya Simba sik hiyo yalifungwa na winga Mkenya, Mark Sirengo mawili, dakika ya tatu na 76 na washambuliaji wazawa, Madaraka Selemani dakika ya 32 na Emanuel Gabriel dakika ya 83, wakati la Yanga lilifungwa na Sekilojo Chambua dk 16.
    Lakini mechi hiyoiliyohudhuriwa na rais mstaafu, marehemu Ali Hassan Mwinyi, chupuchupu ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. 
    Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Abdulkadir alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) ndipo akaendeleza mchezo. 
    Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo na baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa Shirikisho, TFF.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REFA WA ZAMANI MAARUFU NCHINI, OMAR ABDULKADIR AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top