• HABARI MPYA

        Friday, September 13, 2024

        NGUSHI APIGA BAO PEKEE MASHUJAA YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 MWENGE


        BAO la dakika ya 14 la mshambuliaji Crispin Ngushi Mhagmaa limeipa Mashujaa FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), Mwenge Jijini Dar es Salaam.
        Kwa ushindi huo, Mashujaa FC wanafikisha pointi saba na kusogea nafasi ya pili, nyuma ya Singida Black Stars yenye pointi tisa baada ya wote kucheza mechi tatu, wakati Coastal Union inabaki na pointi moja kufuatia kucheza mechi mbili.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: NGUSHI APIGA BAO PEKEE MASHUJAA YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry