// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAXI MPIA NZENGELI APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA COSMO 2-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAXI MPIA NZENGELI APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA COSMO 2-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 06, 2024

    MAXI MPIA NZENGELI APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA COSMO 2-0



    KIUNGO Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli amefunga mabao yote, Yanga ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Cosmopolitan Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),Mwenge Jijini Dar es Salaam. 
    Huo ni mchezo wa pili dhidi ya timu za Daraja la Kwanza ndani ya siku tatu, baada ya juzi Yanga kuichapa Kiluvya United mabao 3-0 hapo hapo KMC siku hiyo mabao yakifungwa na viungo Shekhan Khamis, Salum Abubakar na mshambuliaji mkongo, Jean Baleke.
    Mechi kwa Yanga ni sehemu ya maandalizi ya michezo yao ya Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) ya Ethiopia wakianzia ugenini Septemba 14 Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa, kabla ya kurudiana Uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 20.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXI MPIA NZENGELI APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA COSMO 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top