// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAMA MARIA NYERERE AWAOMBEA DUA WAENDESHA BAISKELI KUMBUKUMBU YA MWALIMU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAMA MARIA NYERERE AWAOMBEA DUA WAENDESHA BAISKELI KUMBUKUMBU YA MWALIMU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 29, 2024

    MAMA MARIA NYERERE AWAOMBEA DUA WAENDESHA BAISKELI KUMBUKUMBU YA MWALIMU


    Na Asha Kigundula, Dar es Salaam
            
    MJANE wa hayati Mwalimu Julius  Nyerere, Mama Maria Nyerere ametoa maombi na dua kwa waendesha baiskeli watakapokuwa safarini kuelekea Butiama.              Akizungumza katika hafla maalum ya kuwaaga wakimbiaji hao 100 iliyofanyika myumbani kwa hayati Julius Kambalage Nyerere, Masaki Jijini Dar es Salaam na ambapo waendesha baiskeli mbele ya Mke wa hayati Mama Maria Nyerere, amewataka wasiache kufanya  maombi ili waweze kufika salama safari yao.                          
    "Nawatakia safari njema, msiache kufanya maombi na Mungu atawasaidia mtafika salama" alisema.                Kufanyika kwa hafla hiyo kiwa ni ishara ya kumuaga tayari kwa kuanza safari kuelekea Butiama ikiwa ni muendelezo wa kumuenzi Baba wa Taifa.         
    Mbio hizo zilizoanza leo jijini Dar asalaam zilisindikizwa na waendesha Baisjeli 200 ambao hao wameishia Msata mkoa wa Pwani, wakiwaacha wenzao 100 ambao wanaelekea Butiama.

                 
    Mkurugenzi Vodacom foundation  Zuwena Farah amesema katika safari hiyo iliyoanza mapema leo Asubuhi, ambapo kituo cha kwanza kilikuwa Msata Mkoani Pwani kwa kupanda miti, kutoa msaada wa Madawati.    "Tumefurahi safari yetu imekuwa na baraka kwa Mama  yetu kipenzi, wakimbiaji wetu watakimbia kwa siku 16 na oktoba 13 watakuwa wamefika butiama kwa ajili ya kufanikisha siku maalum ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa,” alisema.
    Mkuu wa mbio za baiskeli za Twende Butiama, Gabriel Landa,  amesema mbio hizo zitaambatana na utoaji wa huduma kwa jamii zaidi ya afya kama vile kuchangia elimu na kuhamasisha upandaji miti na wanatoa nafasi kwa washiriki zaidi kujiandikisha ili kushiriki kampeni hiyo.
    Akizungumza kwa njaba ya waendesha Baiskeli wenzake, Prince Yakuze amesema anatamani kuona Watanzania wanaenda Burundi kushiriki mashindano ya baiskeli ili kuinua morali kwa waendesha baiskeli nchini huu.          
    Prince Yakuze, raia wa Burundi amesema uwepo wa mashindano mbalimbali ya mchezo wa baiskeli nchini unachangia kuukuza mchezo huo ikilinganishwa  na nchini kwao ambako unaonekana kupoteza mvuto kwenye mchezo huo.
    Zaidi ya waendesha baiskeli 100 wameanza safari hiyo kuelekea Butiama Mara ambapo wanatarajia kufika Oktoba 13 mwaka huu ambapo kilele cha mbio zitafanyika Oktoba 14.              
    Hii ni mara ya sita tangu kuanza kwa safari hiyo ya twende Butiama yenye lengo la kuenzi yaliyowahi kufanywa na baba wa Taifa hayati Mwalimu Julian Nyerere ambaye alifariki miaka 25 iliyopita na kuzikwa nyumbani kwao, Butiama mkoani Mara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAMA MARIA NYERERE AWAOMBEA DUA WAENDESHA BAISKELI KUMBUKUMBU YA MWALIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top