KLABU ya Yanga imemrejesha Kocha Edna Lema ‘Mourinho’ Katika timu ya wanawake, Yanga Princess.
Lema alifanya kazi nzuri Yanga Princess kwa misimu miwili, kabla ya kuachana na timu hiyo mwaka juzi na kwenda kuwa Kocha Msadizi wa timu ya wanaume ya Biashara United ya Mara.
Lakini baada ya juhudi za kujaribu kuirejesha Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Biashara United kukwama msimu uliopita, Lema ameamua kurejea kufundisha wanawake.
0 comments:
Post a Comment