// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KANU KUSHIRIKI KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14 BUTIAMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KANU KUSHIRIKI KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14 BUTIAMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 13, 2024

    KANU KUSHIRIKI KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14 BUTIAMA


    Na Asha Kigundula, Dar es Salaam

    MWANASOKA Bora wa zamani Afrika, Nwankwo Christian Nwosu Kanu atashiriki maazimisho ya miaka 25 ya kifo cha baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania itakayofanyika Oktoba 14, Butiama mkoani Mara.
    Pamoja na Mwanasoka huyo Bora wa Afrika mara mbili, 1996 na 1999, zaidi ya washiriki 100 wamejiandikisha kushiriki mbio za Baiskeli za 'Twende Butiama'  katika kilele cha kumbukumbu ya hayati baba wa Taifa, Mwalimu.
    Kanu, aliyetamba klabu za Iwuanyanwu Nationale ya kwao Nigeria, Ajax ya Uholanzi, Inter Milan ya Italia na Arsenal, West Bromwich Albion na Portsmouth za England - amekuja kwa mwaliko wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya ziara ya mbio za Twende Butiama mwaka 2024. 
    Kupitia taasisi yake ya Kanu Heart Foundation, Kanu ameelezea kufurahishwa kwake kuungana na juhudi zinazofanywa na Twende Butiama kama sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.  
    “Ni fursa ya kipee sana kuwe sehemu ya kuleta mabadiriko kwa jamii hasa katika eneo la afya ambalo linanigusa sana. Upekee huu umenifanya nije Tanzania kuwa mmoja wa washiriki katika ziara hii kwa sababu ni jambo jema,” alisema Kanu katika mkutano na wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 13 Septemba, 2024. 
    Mbio za Twende Butiama zilianzishwa mwaka 2019 na kikundi cha waendesha baiskeli, ili kuadhimisha upendo wa Mwalimu Nyerere wa kuendesha baiskeli na maono yake kimaendeleo katika maeneo matatu muhimu ambayo ni elimu, afya, na utunzaji wa mazingira ambayo yanaweza kuwasaidia Watanzania kupiga hatua kijamii na kiuchumi.
    Mkurugenzi wa Mahusiano na Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah alisema, “Tumefurahi sana Nwankwo Kanu kujumuika nasi katika mbio zetu za Twende Butiama mwaka huu, kwa kushirikiana na taasisi yake ya Moyo tunaamini itatusaidia katika msafara wetu ambapo tunatoa huduma za afya kwa magonjwa yasioambukizwa  katika maeoneo kadha ya mikoa 12 tutakayopita.” 
    Naye mwanzilishi wa mbio za baiskeli za Twende Butiama, Gabriel Landa amesema mbio hizo zitaambatana na utoaji wa huduma kwa jamii zaidi ya afya kama vile kuchangia elimu, na kuhamasisha upandaji miti, na wanatoa nafasi kwa washiriki zaidi kujiandikisha ili kushiriki kampeni hiyo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KANU KUSHIRIKI KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14 BUTIAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top