// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); JKU YAANZA NA MOTO LIGI YA ZENJI, YAITWANGA INTER 3-1 AMAAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE JKU YAANZA NA MOTO LIGI YA ZENJI, YAITWANGA INTER 3-1 AMAAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 06, 2024

    JKU YAANZA NA MOTO LIGI YA ZENJI, YAITWANGA INTER 3-1 AMAAN


    MABINGWA watetezi, JKU wameanza vyema Ligi Kuu ya PBZ Zanzibar baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Inter Zanzibar jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanibar.
    Mabao ya JKU yamefungwa na Koffi Hamza dakika ya saba, Neva Kaboma dakika ya 65 na Tariq Mohammed dakika ya 89, wakati bao pekee la Inter Zanzibar limefungwa na Abdillah Hassan dakika ya 15.
    Ligi Kuu ya PBZ Zanzibar itaendelea kesho kwa mechi nyingine mbili; Mlandege na Chipukizi Uwanja wa New Amaan Complex na Mwenge dhidi ya KVZ Uwanja wa Gombani, Pemba zote zikianza Saa 10:00 jioni.
    Jumapili kutakuwa na mechi mbili pia; Mwembe Makumbi na New City New Amaan Complex na Tekeleza dhidi ya Kipanga Uwanja wa Gombani, zote pia zikianza Saa 10:00 jioni.
    Jumatatu Mafunzo watamenyana na KMKM Uwanja wa Annex A na Uhamiaji dhidi ya Junguni Annex B, wakati Jumanne raundi ya kwanza itakamilishwa kwa mchezo kati ya Malindi na Zimamoto.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKU YAANZA NA MOTO LIGI YA ZENJI, YAITWANGA INTER 3-1 AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top