• HABARI MPYA

        Thursday, September 12, 2024

        DODOMA JIJI YAICHAPA NAMUNGO FC 1-0 BAO LA REKODI YA MSIMU LIGI KUU


        BAO la mshambuliaji Paul Peter sekunde ya 39 dakika ya kwanza limeipa Dodoma Jiji ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Manyara.
        Huo ni ushindi wa kwanza kwa Dodoma Jiji baada ya awali kufungwa 1-0 na Mashujaa mjini Kigoma, kabla ya sare ya bila mabao na Pamba Jijini Mwanza, wakati kwa Namungo imepoteza mechi ya tatu mfululizo – pamoja na zile mbili za nyumbani ilizofungwa 2-1 na Tabora United na 2-0 na Fountain Gate huko Ruangwa.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA NAMUNGO FC 1-0 BAO LA REKODI YA MSIMU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry