// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO NA KLABU YA AIK YA SWEDEN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO NA KLABU YA AIK YA SWEDEN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 06, 2024

    AZAM FC YAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO NA KLABU YA AIK YA SWEDEN


    KLABU ya imepiga hatua kwa kutanua wigo wake wa kuwa klabu bora nchini na Afrika kwa ujumla baada ya leo kuingia mkataba wa miaka mitano na Klabu ya AIK Football ya Sweden.
    Mkataba huo utakaodumu hadi mwaka 2029, una lengo la kutoa nafasi kwa wachezaji wa kituo cha kukuzia vipaji cha Azam FC kufanya mazoezi na kuendelezwa katika kituo cha kukuza vipaji cha AIK Football.
    Kupitia mkataba huo, wachezaji watakaofanya vizuri katika kituo cha kukuzia vipaji cha Azam FC, watapata nafasi ya kwenda Stockholm, Sweden kufanya mazoezi na AIK Football. 
    Wakiwa Sweden, wachezaji wa Azam FC watapata mafunzo chini ya wataalam waliobobea na wale watakaofanya vizuri watajiunga na kikosi cha kwanza cha timu ya AIK Football bila kusubiri mlolongo mrefu.
    Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Omary Kuwe amesema mkataba huu unatoa nafasi kwa wachezaji chipukizi wa Azam FC kutimiza ndoto zao za kucheza Ulaya.
    Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa AIK Football, Fredrik Soderberg amesema amefurahishwa na ushirikiano wao walioingia mkataba kwani utaiwezesha timu yao kupata vipaji kutoka Azam FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO NA KLABU YA AIK YA SWEDEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top