// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 22, 2024

    AZAM FC YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 CHAMAZI


    WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Bao pekee la Azam FC limefungwa na mshambuliaji Nassor Saadun Hamoud dakika ya tisa baada ya kuwachambua beki Lameck Lawi na kipa wake, Mkongo Leyi Matampi.
    Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi nane katika mchezo wa nne, wakati Coastal Union inabaki na pointi yake moja baada ya kucheza mechi nne pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top