// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAACHANA NA KOCHA DABO BAADA YA MIEZI 15 TANGU AWASILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAACHANA NA KOCHA DABO BAADA YA MIEZI 15 TANGU AWASILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, September 03, 2024

    AZAM FC YAACHANA NA KOCHA DABO BAADA YA MIEZI 15 TANGU AWASILI


    KLABU ya Azam FC imeachana na kocha wake Msenegal, Youssoupha Dabo (44) baada ya miezi 15 ya kuwa kazini tangu awasili kutoka ASC Jaraaf ya kwao.
    Uamuzi huu unafuatia mwanzo mbaya wa msimu kwa Azam FC, ikifungwa 4-1 na Yanga katika Fainali ya Ngao ya Jamii, kabla ya kutolewa na APR katika Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika, ikichapwa 2-0 Kigali baada ya kushinda 1-0 Dar es Salaam.
    Aidha, Azam FC iliambulia sare ya bila mabao na wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wao wa kwanza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, matokeo ambayo yalifuatiwa na tetesi na kocha Dabo kuondolewa kazini.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAACHANA NA KOCHA DABO BAADA YA MIEZI 15 TANGU AWASILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top