KLABU ya Azam FC imetambulisha benchi jipya la Ufundi chini ya Kocha Mkuu Mmoroco, Rachid Taoussi (65) mwenye uzoefu wa kufundisha kuanzia mwaka 1992.
Taoussi anajiunga na Azam FC kwa Mkataba wa mwaka mmoja kwa pamoja na wasaidizi wake watatu, Kocha Msaidizi, Ouajou Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Badr Eddine na Kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui wote Wamorocco.
0 comments:
Post a Comment