// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA YATOKA NYUMA NA KUICHAPA RED ARROWS 2-1 DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA YATOKA NYUMA NA KUICHAPA RED ARROWS 2-1 DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, August 04, 2024

    YANGA YATOKA NYUMA NA KUICHAPA RED ARROWS 2-1 DAR


    TIMU ya Yanga imetoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa kirafiki leo kuhitimisha tamasha la kilele cha Wiki ya Mwananchi usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Red Arrows, mabingwa wa mwaka huu Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati walitangulia kwa bao la mshambuliaji Ricky Banda dakika ya sita, kabla ya viungo, mzawa Mudathir Yahya Abbas kusawazisha dakika ya 62 na Mburkinabe Stephane Aziz Ki kufunga la ushindi dakika ya 90’+3 kwa penaltı.
    Huo unakuwa mchezo wa nne kwa Yanga katika maandalizi yake ya msimu mpya baada ya awali kucheza mechi tatu kwenye kambi yake ya Afrika Kusini, ikishinda 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs na 1-0 dhidi ya TS Galaxy kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mechi ya kwanza na Augsburg ya Ujerumani.
    Yanga sasa inarejea kambini Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 8 hapo hapo Uwanja wa Mkapa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YATOKA NYUMA NA KUICHAPA RED ARROWS 2-1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top