MABINGWA wa Tanzania, Yanga wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kutoka nyuma na kushinda mabao 4-1 dhidi ya Azam FC usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Azam FC walitangulia kwa bao la kiungo mzawa Feisal Salum dakika ya 13, akimalizia krosi ya winga Mgambia, Gibril Sillah kutoka kulia kumchambua kipa namba moja wa Mali, Djigui Diarra.
Yanga ikazinduka kwa mabao ya mshambuliaji Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 19, beki Mmali, Yoro Mamadou Diaby aliyejifunga dakika ya 28, kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 31 na mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize dakika ya 90’+1.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, bao Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 11 liliipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union hapo hapo Uwanja wa Benjamin Mkapa.
0 comments:
Post a Comment