KLABU ya Simba imemtambulisha mlindamlango Moussa Camara (25) kuwa mchezaji wake mpya wa 15 kuelekea msimu ujao kutoka Horoya ya kwao, Guinea.
Huo ni usajili wa dharula kufuatia Kipa wa kwanza wa sasa Simba, Mmorocco Ayoub Lekred kuumia huku kipa mwingine, Aishi Manula akiripotiwa kugoma kwenda kambini.
Wachezaji wengine 14 waliosajiliwa Simba ni mabeki, Kelvin Sospeter Kijiri (24) kutoka Singida Big Stars, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya (DRC), wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
Wengine ni viungo, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, Awesu Ally Awesu (27) kutoka KMC, Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma, Yusuph Ally Kagoma (28) kutoka Singida Big Stars, Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe, Débora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia.
Kuna washambuliaji pia, Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.
Simba pia imeajiri Kocha mpya Mkuu, Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids ambaye amekuja na safu yake nzima ya Wasaisizi, wote raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee.
0 comments:
Post a Comment