// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA QUEENS YATUPWA NJE LİGİ YA MABINGWA AFRİKA CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA QUEENS YATUPWA NJE LİGİ YA MABINGWA AFRİKA CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, August 26, 2024

    SIMBA QUEENS YATUPWA NJE LİGİ YA MABINGWA AFRİKA CECAFA


    TIMU ya Simba Queens imetupwa nje ya kinyang’anyiro cha tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Polisi Bullets ya Kenya leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa, Ethiopia.
    Mabao ya Polisi yamefungwa na Lucy Kwekwe dakika ya 29, Diana Wacera dakika ya 60 na Rebecca Okwaro dakika ya 82, wakati ya Simba Queens yote yamefungwa na kiungo Mkenya, Vivian Corazone Aquino Odhiambo.
    Sasa Polisi itamenyana na wenyeji, CBE katika Fainali Jumatano, ambao wameitoa Kawempe Muslim ya Uganda kwa kuichapa mabao 2-1 leo pia.
    Simba Queens itawania nafasi ya tatu dhidi ya Kawempe katika mchezo wa utangulizi Jumatano. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA QUEENS YATUPWA NJE LİGİ YA MABINGWA AFRİKA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top