TIMU ya Pamba Jiji FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Hiyo inakuwa suluhu ya pili mfululizo nyumbani kwa Pamba iliyorejea Ligi Kuu msimu huu kufuatia kutoka sare ya 0-0 pia katika mchezo wa kwanza na Tanzania Prisons hapo hapo Kirumba.
0 comments:
Post a Comment