TIMU ya Pamba Jiji FC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Vital'O ya Burundi katika mchezo wa kirafiki kuhitimisha tamasha la Pamba Day leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Pamba Jiji FC iliyopanda Ligi Kuu yaNBC Tanzania Bara msimu huu ilitangulia kwa bao la mshambuliaji Mghana, Erick Okutu dakika ya 55, kabla ya kiungo Hakizimana Ramadhani kuisawazishia Vital'O kwa penalti dakika ya 79.
0 comments:
Post a Comment