// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGUSHI AFUNGA BAO PEKEE MASHUJAA YAILAZA DODOMA JIJI 1-0 KIGOMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGUSHI AFUNGA BAO PEKEE MASHUJAA YAILAZA DODOMA JIJI 1-0 KIGOMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 17, 2024

    NGUSHI AFUNGA BAO PEKEE MASHUJAA YAILAZA DODOMA JIJI 1-0 KIGOMA


    BAO pekee la mshambuliaji Crispin Ngushi Mhagama dakika ya 33 limeipa Mashujaa FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
    Ushindi huo katika mchezo wao wa kwanza wa msimu unawafanya Mashujaa FC waanzie kileleni mwa Ligi Kuu, kufuatia timu za Pamba na Tanzania Prisons kutoka sare ya bila kufungana jana Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Mchezo mwingine uliokuwa ufanyike leo usiku baina ya Namungo FC na Fountain Gate umeahirishwa kutokana na klabu kutokamilisha taratibu muhimu za usajili.
    Mechi nyingine mbili zitafuatia kesho, Saa 8:00 mchana Ken Gold wataumana na Singida Black Stars Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya – na baadaye Saa 10:15 jioni, vigogo, Simba watamenyana na Tabora United Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGUSHI AFUNGA BAO PEKEE MASHUJAA YAILAZA DODOMA JIJI 1-0 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top