MWANAMICHEZO wa tatu wa Tanzania, Sophia Anisa Latiff Jumamosi alitupwa nje kwenye Michezo ya Olimpiki kufuatia kumaliza wa mwisho katika waogeleaji nane mita 50 (Freestyle) kwa wanawake akitumia muda wa sekunde 28:42 na kuweka rekodi mpya binafsi.
Mshindi, Jovana Kuljaca wa Montenegro alitumia sekunde 27:19 na wa pili Christina Rach wa Dubai akitumia sekunde 27:20, huku Kennice Aphenie Greene wa St Vincent & the Grenadines akimalza wa tatu kwa kutumia sekunde 27:23.
Sophia anamfuatia muogeleaji mwenzake wa Tanzania, Collins Phillip Saliboko aliyetolewa katika mita 100 (Freestyle) kwa wanaume Julai 30 baada ya kumaliza katika nafasi ya saba akitumia sekunde 53:38, wakati mshindi wa kwanza Ovesh Purahoo wa Mauritius alitumia sekunde 52:22, ikiwa ni tofauti ya sekunde 1:16 tu.
Sasa matumaini ya Watanzania kwenye Michezo hiyo inayoendelea Jijini Paris yamebaki kwa wanariadha wanne wa mbio ndefu pekee, Alphonce Felix Simbu na Gabriel Geay, wanaume na Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri wanawake.

0 comments:
Post a Comment