// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAXI MPIA NZENGELI AIPELEKA YANGA FAINALI NGAO YA JAMII...MNYAMA CHALI ILE YENYEWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAXI MPIA NZENGELI AIPELEKA YANGA FAINALI NGAO YA JAMII...MNYAMA CHALI ILE YENYEWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, August 08, 2024

    MAXI MPIA NZENGELI AIPELEKA YANGA FAINALI NGAO YA JAMII...MNYAMA CHALI ILE YENYEWE


    KLABU ya Yanga imefanikiwa kutinga Fainali ya Ngao ya Jamii kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya watani, Simba katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 44 akimalizia pasi nzuri ya mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo.
    Sasa Yanga watakutana na Azam FC katika Fainali itakayopigwa Jumapili hapo hapo Uwanja wa Mkapa kuanzia Saa 1:00 usiku ikitanguliwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu itakayoanza Saa 10:00 jioni.
    Azam FC imetinga Fainali kwa ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Mabao ya Azam yamefungwa na winga Mgambia Gibril Sillah dakika ya 13, kiungo Feisal Salum dakika ya 40, washambuliaji Mcolombia Jhonier Blanco dakika ya 45'+1, Adam Omary dakika ya 87 na kiungo Mcolombia, Ever William Meza Mercado dakika ya 90'+2.
    Kwa upande wao, Coastal Union ambayo itakutana na Simba Jumapili jioni, mabao yao yamefungwa na kiungo Charles Semfuko dakika ya 27 na  Abdallah Hassan dakika ya 85.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXI MPIA NZENGELI AIPELEKA YANGA FAINALI NGAO YA JAMII...MNYAMA CHALI ILE YENYEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top