// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KOCHA AZAM ASEMA MECHI ITAKUWA NGUMU, LAKINI WATAPAMBANIA USHINDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KOCHA AZAM ASEMA MECHI ITAKUWA NGUMU, LAKINI WATAPAMBANIA USHINDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 10, 2024

    KOCHA AZAM ASEMA MECHI ITAKUWA NGUMU, LAKINI WATAPAMBANIA USHINDI


    KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Mfaransa Bruno Ferry amesema mechi ya Fainali ya Ngao ya Jamii kesho dhidi ya Yanga kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam itakuwa ngumu, lakini wamejipanga kushinda ili kuuanza msimu na taji hilo.
    Akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Ferry amesema Yanga na timu nzuri na siku zote mechi dhidi yao zimekuwa ngumu.
    "Msimu uliopita tulitolewa katika Nusu Fainali, inamaanisha msimu huu tumepiga hatua katika mipango yetu, ni vizuri kucheza Fainali. Kucheza na timu kama Yanga, kutakuwa na mashabiki wengi uwanjani, nafikiri ni mchezo ambao tutaufurahia, nafikirinutakuwa mchezo mgumu,"amesema Ferry na kuongeza;
    "Nafikiri sihitaji kuzungumza zaidi kuhusu timu ya Yanga, kila mtu anajua ni timu bora mno, na uwezo binafsi wa wachezaji wake ni mkubwa, wameimarika zaidi ya msimu uliopita, hivyo kwetu ushindani ni mkubwa,"amesema.
    Hata hivyo, Ferry amesema wamekuwa na maandalizi mazuri tangu mwanzo wa msimu na kwa kufika Fainali basi watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri dhidi ya Yanga kesho. 
    Azam FC wameingia Fainali baada ya kuitoa Coastal Union kwa kuichapa mabao 5-2 juzi Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar - wakati Yanga iliwachapa watani, Simba SC 1-0 juzi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Mchezo huo utatanguliwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu baina ya Coastal Union na Simba SC kuanzia Saa 10:00 jioni.
    Mara ya mwisho timu hizo zilikutana Juni 2, mwaka huu katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la CRDB na Yanga ikaibuka na ushindi wa penalti 6-5 kufuatia sare ya bila mabao ndani ya dakika 120 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. 
    Msimu uliopita kwenye Ngao ya Jamii timu hizo zilikutana katika Nusu Fainali Agosti 9, mwaka jana na Yanga ikaichapa Azam FC 2-0, mabao ya Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na Clement John Mzize dakika ya 89 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Hata hivyo, ni Simba iliyotwaa taji hilo kwa kuifunga kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga Agosti 13, mwaka jana.
    Mechi mbili za Ligi Kuu msimu uliopita kila timu ilishinda moja, Oktoba 23, mwaka jana Stephane Aziz Ki alifunga mabao yote ya Yanga ikishinda 3-2 Uwanja Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam - huku mabao ya Azam yakifungwa Gibrill Sillah na Prince Dube Mpumelelo aliyehamia Jangwani.
    Machi 17, mwaka huu mabao ya Gibrill Sillah dakika ya 19 na Feisal Salum Abdallah dakika ya 51 yaliipa Azam FC ushindi wa 2-1 dhidi ya Yanga ambayo ilitangulia kwa bao la Clement Francis Mzize dakika ya 10.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA AZAM ASEMA MECHI ITAKUWA NGUMU, LAKINI WATAPAMBANIA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top