// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HERI SASII REFA WA SIMBA NA YANGA KESHOKUTWA DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HERI SASII REFA WA SIMBA NA YANGA KESHOKUTWA DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 06, 2024

    HERI SASII REFA WA SIMBA NA YANGA KESHOKUTWA DAR


    REFA Heri Sasii ndiye atakayechezesha mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga katika Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii Alhamisi kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Sasii atasaidiwa na Washika Vibendera, Kassim Mpanga, wote wa wa Dar es Salaam na Mohamed Mkono wa Tanga, wakati mezani atakuwepo Amina Kyando wa Morogoro na Mtathmini wa mchezo ni Refa Mstaafu wa FIFA, Soud Abdi wa Arusha.
    Naye Refa Bora wa Msimu, Ahmed Arajiga wa Manyara atachezesha Nusu Fainali nyingine kati ya Azam FC na Coastal Union Alhamisi kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Arajiga atasaidiwa na Janeth Balama wa Iringa na Ally Ramadhani wa Zanzibar, wakati mezani atakuwepo Nasri Siyah wa Zanzibar na Mtathmini wa mchezo huo ni refa mstaafu wa FIFA, Victror Mwandike wa Mtwara. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HERI SASII REFA WA SIMBA NA YANGA KESHOKUTWA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top