MSHAMBULIAJI Mnorway, Erling Braut Haaland jana amefunga mabao matatu kuiwezesha Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ipswich Town katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Kiungo wa Kimataifa wa Jamhuri ya Ireland, Samuel Joseph Szmodics alianza kuifungia Ipswich Town dakika ya saba, kabla ya Haaland kuisawazishia Man City kwa penalti dakika ya 12.
Kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne akaifungia Man City bao la pili dakika ya 14, kabla ya Haaland kuongeza mawili dakika ya 16 na 88, huo ukiwa ushindi wa pili katika mechi mbili za mwanzo za msimu, kufuatia kuwachapa Chelsea 2-0 Jijini London.
Kwa Ipswich Town iliyopanda msimu huu hicho ni kipigo cha pili kufuatia kuchapwa 2-0 na Liverpool kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Uwanja wa Portman Road mjini Ipswich, Suffolk.
0 comments:
Post a Comment