// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DEBORA AFUNGA BAO ZURI SIMBA YAICHAPA APR 2-0 KIGALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DEBORA AFUNGA BAO ZURI SIMBA YAICHAPA APR 2-0 KIGALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 03, 2024

    DEBORA AFUNGA BAO ZURI SIMBA YAICHAPA APR 2-0 KIGALI


    TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya APR ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki kuhitimisha tamasha la 16 la Simba Day usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC jana yalifungwa na kiungo mpya mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola aliyesajiliwa kutoka Mutondo Stars ya Zambia, Debora Fernandez Mavambo dakika ya 46 na mshambuliaji, Edwin Charles Balua dakika ya 66.
    Huo unakuwa mchezo wa nne mfululizo Simba inashinda chini ya Kocha mpya, Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids anayesaidiwa na raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee. 
    Awali katika kambi ya mjini Ismailia nchini Misri – Simba ilishinda 3-0 dhidi ya El-Qanah Julai 22 na 2-1 mara mbili, dhidi ya Telecom Egypt Julai 28 na dhidi ya Al-Adalah FC ya Saudi Arabia Julai 29.
    Simba sasa inarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani, Yanga Agosti 8 Uwanja wa Mkapa.
    GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DEBORA AFUNGA BAO ZURI SIMBA YAICHAPA APR 2-0 KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top