// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); COASTAL UNION YAWACHAPA UHAMIAJI 2-0 MECHI YA KIRAFIKI ZANZIBAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE COASTAL UNION YAWACHAPA UHAMIAJI 2-0 MECHI YA KIRAFIKI ZANZIBAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 06, 2024

    COASTAL UNION YAWACHAPA UHAMIAJI 2-0 MECHI YA KIRAFIKI ZANZIBAR


    TIMU ya Coastal Union jana iliibuka na ushind wa 2-0 dhidi ya washiriki wenzao wa Kombe la Shirikisho Afrika, Uhamiaji Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Mabao ya Coastal Union katika mchezo huo wa kuhitimisha maandalizi ya msimu yalifungwa na Abdallah Hassan na Denis Modzaka. 
    Awali Coastal Union iliweka kambi ya wiki moja Tanga baada ya kutolewa mapema kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Jijini Dar es Salaam – kabla ya kwenda Pemba ambako waliweka kambi ya wiki mbili na ushei.
    Coastal Union inatarajiwa kushuka Uwanja wa New Amaan Complex keshokutwa Saa 10:00 jioni kumenyana na Azam FC katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YAWACHAPA UHAMIAJI 2-0 MECHI YA KIRAFIKI ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top