KLABU zote zinazoshiriki Hatua za Awali za michano ya Afrika, Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa kila moja itapata ruzuku ya dola za Kimarekani 50,000, zaidi ya Sh. Milioni 135 za Tanzania kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF leo, hiyo ni sehemu ya ahadi ya Rais wa Shirikisho hilo la kandanda barani, Dk Patrice Motsepe kuboresha michuano hiyo kwa kutoa misaada zaidi ya kifedha kwa klabu.
Raundi ya Kwanza ya Awali michuano ya Afrika inaanza leo kwa mechi za mkondo wa kwanza na marudiano yatafutaia Agosti 23 hadi 25, mwaka huu, wakati Raundi ya Pili itafuatia Septemba, kabla ya hatuanya makundi.
Wanufaika wa fedha kwa Tanzania ni klabu za Azam, Yanga Ligi ya Mabingwa na Coastal Union na Simba katika Kombe la Shirikisho. Azam, Yanga na Coastal zinaanzia Raundi ya Awali, wakati Simba itaanzia Raundi ya kwanza.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa CAF kutoa msaada wa kifedha kwa klabu katika hatua ya Awali , kwani ruzuku na zawadi zimekuwa zikitoka kuanzia Hatua za Makundi.
Tayari CAF imeboresha zawadi za washindi wa michuano hiyo zawadi ya mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa ikipanda kutoka dola Milioni 2.5 hadi Milioni 4 za mwaka 2022, wakati mshindi wa Kombe la Shirikisho anapata Dola Milioni 2 kutoka Dola 1.2 mwaka 2022.
Mwaka jana CAF ilifanya michuano ya Ligi ya Klabu Afrika (AFC), ambayo klabu zilivuna jumla ya dola Milioni 8.
ZAWADI ZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
Bingwa: Dola 4,000,000
Mshindi wa Pili: Dola 2,000,000
Nusu Fainali: Dola 1,200,000
Robo Fainali: Dola 900,000
Nafasi ya Tatu kwenye Kundi: Dola 700,000
Nafasi ya Nne kwenye Kundi: Dola 700,000
ZAWADI ZA KOMBE LA SHIRIKISHO:
Bingwa: Dola 2,000,000
Mshindi wa Pili: Dola 1,000,000
Nusu Fainali: Dola 750,000
Robo Fainali: Dola 550,000
Nafasi ya Tatu kwenye Kundi: Dola 400,000
Nafasi ya Nne kwenye Kundi: Dola 400,000

0 comments:
Post a Comment