// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YATOLEWA, APR WAISUBIRI PYRAMIDS KUWANIA MAKUNDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YATOLEWA, APR WAISUBIRI PYRAMIDS KUWANIA MAKUNDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 24, 2024

    AZAM FC YATOLEWA, APR WAISUBIRI PYRAMIDS KUWANIA MAKUNDI


    SAFARI ya Azam FC katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imeishia mwanzoni tu baada ya leo kutolewa na wenyeji, APR kufuatia kuchapwa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali nchini Rwanda.
    Mabao ya APR yamefungwa na kiungo Jean Bosco Ruboneka dakika ya 45 na mshambuliaji Gilbert Mugisha dakika ya 62 na kwa matokeo hayo Azam FC iliyoshinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza wiki iliyopita Dar es Salaam inatolewa kwa kipigo cha jumla cha 2-1.
    Sasa APR inaweza kukutana na Pyramids ya Misri ambayo inarudiana na JKU leo nchini Misri ikiwa na mtaji wa ushindi wa 6-0 kwenye mechi ya kwanza ambayo kama ya leo ilichezwa Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YATOLEWA, APR WAISUBIRI PYRAMIDS KUWANIA MAKUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top