// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAIFUATA APR USIKU HUU SHUGHULI NI JUMAMOSI AMAHORO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAIFUATA APR USIKU HUU SHUGHULI NI JUMAMOSI AMAHORO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, August 21, 2024

    AZAM FC YAIFUATA APR USIKU HUU SHUGHULI NI JUMAMOSI AMAHORO


    KIKOSI cha Azam FC kinatarajiwa kuondoka Saa 9 usiku wa leo kwenda Kigali, nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, APR Jumamosi Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali.
    Afisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria 'Zaka Zakazi' amesema timu inaondoka na wachezaji 22, huku wengine wakikosekana kwenye safari hiyo kipa Ali Ahamada, viungo Yahya Zayd, Sospter Bajana, Abdul Khamis Suleiman 'Sopu' na washambuliaji, Msenegal Alassane Diao na Mcolombia, Franklin Navarro kwa sababu ni majeruhi.
    Ikumbukwe mchezo wa kwanza Azam FC iliibuka na ushindi wa 1-0 bao pekee la mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco Yus dakika ya 56 kwa penalti kufuatia kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari Jumapili. 
    Mshindi wa jumla kati ya Azam ma APR atakutana na mshindi wa jumla kati ya JKU na Pyramids ya Mısri kuwania kuingia hatua ya makundi, 16 Bora.
    Pyramids iliichapa JKU 6-0 juzi Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo na marudiano yao ni Jumamosi pia hapo hapo Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAIFUATA APR USIKU HUU SHUGHULI NI JUMAMOSI AMAHORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top