TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Rayon Sport katika mchezo wa kirafiki leo na kutwaa taji la Choplife Cup 2024 Uwanja wa Pele Kigali, Nyamirambo nchini Rwanda.
Bao pekee la Azam FC leo limefungwa na beki, Lusajo Elukaga Mwaikenda dakika ya 57 na huo unakuwa mchezo wa tano kwa Azam FC katika maandalizi ya msimu mpya.
Awali ilishinda 4-0 dhidi ya wenyeji, Zimamoto Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar Julai 12, kabla ya kwenda kushinda 3-0 Julai 20 dhidi ya Union Yacoub El Mansour, kutoa sare ya 1-1 na Union de Touarga Julai 27, kabla ya kuchapwa 4-1 na Wydad Athletic FC Julai 29 katika kambi yao ya Morocco.
Azam FC sasa wanarejea nyumbani na kupitiliza Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii Agosti 8 Uwanja wa New Amaan Complex.

0 comments:
Post a Comment