// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ARAJIGA APEWA AZAM NA YANGA, KAYOKO COASTAL NA SIMBA KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ARAJIGA APEWA AZAM NA YANGA, KAYOKO COASTAL NA SIMBA KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, August 10, 2024

    ARAJIGA APEWA AZAM NA YANGA, KAYOKO COASTAL NA SIMBA KESHO


    REFA mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Ahmed Arajiga ndiye atakayechezesha Fainali ya Ngao ya Jamii baina ya Azam FC na Yanga SC kesho kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Arajiga Refa Bora wa msimu atasaidiwa na Frank Komba wa Dar es Salaam na Mohamed Mkono wa Tanga, wakati mezani atakuwepo Amina Kyando wa Morogoro na Mtathmini wa mchezo ni Refa Mstaafu wa FIFA, Soud Abdi wa Arusha.
    Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu baina ya Coastal Union na Simba utakaochezwa kesho Saa 10:00 jioni hapo hapo Uwanja wa Mkapa utachezeshwa na Ramadhani Kayoko atakayesaidiwa na Glory Tesha, wote wa Dar es Dalaam na Hamdan Said wa Mtwara.
    Refa wa akiba kwenye mchezo huo atakuwa Isihaka Mwalile wa Dar es Salaam na Mtathmini wa mechi hiyo ni Refa Mstaafu wa FIFA pia, Isaro Chacha wa Mwanza.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARAJIGA APEWA AZAM NA YANGA, KAYOKO COASTAL NA SIMBA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top