Thursday, August 08, 2024

    ADA YA MCHEZAJI WA KIGENI BARA SASA NI SHILINGI MILIONI 8 KWA MSIMU


    ADA ya mchezaji wa kigeni kwa msimu katika Ligi Kuu ya NBC, Championship na Daraja la Kwanza Tanzania Bara imepanda kutoka Sh. Milioni 4 za msimu uliopita hadi Sh. Milioni 8 kuanzia msimu huu.
    Kwa mujibu kanuni mpya za Ligi hiyo zilizotolewa na Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB), idadi ya wachezaji wa kigeni haijabadilika.
    Aidha, Bodi imeruhusu rasmi timu za Bara kupeleka mechi zake visiwani Zanzibar na kutangaza rasmi kuanzia msimu huu kutakuwa na Ligi ya Muungano, ambayo itashirkisha timu mbili za kila upande, Bara na visiwani.
    GONGA KUSOMA ZAIDI KANUNI MPYA ZA LIGI KUU
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ADA YA MCHEZAJI WA KIGENI BARA SASA NI SHILINGI MILIONI 8 KWA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry