KIKOSI cha Yanga kimewasili salama jana nchini Afrika Kusini kwa kambi ya kujiandaa na msimu itakayoambatana na mechi kadhaa za kirafiki.
Mabingwa hao wa Tanzania wataanza kwa kumenyana na Augsburg ya Ujerumani Jumamosi Uwanja wa Mbombela, Mpumalanga, kabla ya kucheza na wenyeji, TS Galaxy Julai 24 katika mchezo ambao hautakuwa na mashabiki.
Yanga itakamilisha zara yake kwa mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya wenyeji wengine, Kaizer Chiefs Julai 28 Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein.
Akizungumza wakati wa safari hiyo, kocha Mkuu wa Yanga, Muargentina Miguel Angel Gamondi amesema kwamba ameridhishwa na namna wachezaji wapya wanavyoendelea kuelewana na wenzao.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea nchini Julai 30 tayari kwa tamasha la kilele cha wiki ya Mwananchi Agosti 4 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya kumenyana na watani, Simba katika Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii Agosti 8.

0 comments:
Post a Comment