// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC KWENDA AFRİKA KUSINI KESHO KUCHEZA NA TIMU YA BUNDESLIGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC KWENDA AFRİKA KUSINI KESHO KUCHEZA NA TIMU YA BUNDESLIGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, July 17, 2024

    YANGA SC KWENDA AFRİKA KUSINI KESHO KUCHEZA NA TIMU YA BUNDESLIGA


    KIKOSI cha Yanga kinatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Afrika Kusini kwa ziara ya mechi kadhaa za kirafiki, ikiwemo dhidi ya Augsburg inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani.
    Yanga watamenyana na timu hiyo ya Bundesliga Jumamosi wiki hii kuanzia Saa 10:00 jioni kwenye michuano ya Mpunalanga Premier’s International Cup 2024.
    Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ni kwamba wamealikwa na klabu ya TS Galaxy ya Afrika Kusini ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini kucheza michuano hiyo.
    Tayari Yanga ina mwaliko mwingine wa Afrika Kusini kwenye michuano mipya ya Kombe la Toyota na watamenyana na wenyeji wao, Kaizer Chiefs Julai nchini humo Saa 10:00 jioni pia.
    Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea nchini Julai 30 tayari kwa tamasha la kilele cha wiki ya Mwananchi Agosti 4 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Ikumbukwe Yanga itauanza msimu kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya mtani, Simba SC Agosti 8.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC KWENDA AFRİKA KUSINI KESHO KUCHEZA NA TIMU YA BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top