• HABARI MPYA

        Thursday, July 04, 2024

        TAIFA STARS YAPANGWA NA DRC, GUINEA NA ETHIOPIA KUWANIA TIKETI YA AFCON 2025

        TANZANIA imepangwa Kundi H pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Guinea na Ethiopia kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Morocco mwaka 2025.
        Katika Droo iliyopangwa leo Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, mabingwa watetezi, Ivory Coast wamepangwa Kundi G pamoja na Zambia, Sierra Leone na Chad.
        Jumla ya nchi 52 zinatarajiwa kushiriki hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya AFCON 2025 kuanzia Septemba 2 hadi Novemba 19 mwaka huu na washindi wawili wa makundi yote 12 watatengeneza idadi ya timu 24 wakiwemo wenyeji Morocco, kufuzu AFCON ya mwakani.

        MAKUNDI YOTE KUFUZU AFCON 2025 MOROCCO
        Kundi A: Tunisia, Madagascar, Comoros, Gambia
        Kundi B: Morocco, Gabon,Central Africa Republic, Lesotho 
        Kundi C: Egypt, Cape Verde, Mauritania, Botswana
        Kundi D: Nigeria, Benin Libya, Rwanda 
        Kundi E: Algeria, Equatorial Guinea, Togo, Liberia
        Kundi F: Ghana, Angola, Sudan, Niger
        Kundi G: Cote d'Ivoire, Zambia, Sierra Leone, Chad
        Kundi H: DR Congo, Guinea, Tanzania, Ethiopia
        Kundi I: Mali, Mozambique, Guinea Bissau, Eswatini
        Kundi J: Cameroon, Namibia, Kenya, Zimbabwe
        Kundi K: South Africa, Uganda, Congo, South Sudan
        Kundi L: Senegal, Burkina Faso, Malawi, Burundi


        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: TAIFA STARS YAPANGWA NA DRC, GUINEA NA ETHIOPIA KUWANIA TIKETI YA AFCON 2025 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry