// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SINGIDA BIG STARS YAPIGWA TENA, YACHAPWA 3-1 NA SC VILLA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SINGIDA BIG STARS YAPIGWA TENA, YACHAPWA 3-1 NA SC VILLA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, July 12, 2024

    SINGIDA BIG STARS YAPIGWA TENA, YACHAPWA 3-1 NA SC VILLA


    TIMU ya Singida Big Stars imejiweka kwenye nafasi ngumu ya kusonga mbele michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya kuchapwa mabao 3-1 na SC Villa ya Uganda katika mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya SC Villa yamefungwa na Njib Yiga dakika ya 45’+1, Patrick Kakande dakika ya 52 na Reagan Mpande dakika ya 56, wakati bao pekee la Singida Big Stars limefungwa na Marouf Tchakei dakika ya 61.
    SC Villa inafikisha pointi nne kufuatia sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini, wakati Singida Big Stars inafikisha mechi mbili bila ushindi kufuatia kuchapwa 1-0 na APR ya Rwanda katika mchezo wa kwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAPIGWA TENA, YACHAPWA 3-1 NA SC VILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top