TIMU ya Simba SC imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Telecom Egypt katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mercure kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya mjini Ismailia nchini Misri.
Mabao ya Simba leo yamefungwa na mshambuliaji mpya, Valentino Mashaka Kusengama aliyesajiliwa kutoka Geita Gold na Ladaki Juma Chasambi.
Huo unakuwa mchezo wa pili kwenye kambi yao hiyo baada ya Julai 22 kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya El-Qanah, mabao ya viungo, Muivory Coast Jean Charles Ahoua mawili, dakika ya 14 na 16 na Mnigeria, Augustine Okejepha dakika ya 120.
Simba SC imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mjini Ismailia nchini Mısri na inatarajiwa kurejea nchini mapema Agosti kwa ajili ya tamasha la Simba Day Agosti 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Baada ya hapo Simba itarejea Uwanja wa Mkapa Agosti 8 kumenyana na watani, Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.
0 comments:
Post a Comment