// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YAICHAPA 2-1 TIMU YA SAUDI ARABIA MECHI YA KIRAFIKI MISRI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YAICHAPA 2-1 TIMU YA SAUDI ARABIA MECHI YA KIRAFIKI MISRI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, July 29, 2024

    SIMBA SC YAICHAPA 2-1 TIMU YA SAUDI ARABIA MECHI YA KIRAFIKI MISRI


    TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al-Adalah FC ya Saudi Arabia katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri.
    Mabao ya Simba SC inayofundishwa na Kocha Fadluraghman "Fadlu" Davids raia wa Afrika Kusini yamefungwa na washambuliaji wapya, Mganda Steven Mukwala dakika ya tisa na Mzambia, Joshua Mutale dakika ya 32.
    Huo unakuwa mchezo wa tatu kwa Simba SC kwenye kambi yao hiyo baada ya Julai 22 kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya El-Qanah na jana kushinda 2-1 dhidi ya Telecom Egypt  Uwanja wa Mercure kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya mjini Ismailia nchini Misri.
    Simba SC imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mjini Ismailia nchini Mısri na inatarajiwa kurejea nchini mapema Agosti kwa ajili ya tamasha la Simba Day Agosti 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Baada ya hapo Simba itarejea Uwanja wa Mkapa Agosti 8 kumenyana na watani, Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA 2-1 TIMU YA SAUDI ARABIA MECHI YA KIRAFIKI MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top