MECHI za Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii zitachezwa Agosti 8, Azam FC dhidi ya Coastal Union kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na Simba dhidi ya Yanga kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mechi zote za mwisho zitachezwa Agosti 11, ikitangulia ya kusaka mshindi wa tatu Saa 9:00 Alasiri na kufuatiwa na Fainali Saa 1:00 Usiku.
Mfumo wa timu nne katika Ngao ya Jamii ulianza rasmi msimu uliopita kwa bingwa wa Ligi Kuu kucheza na mshindi wa tatu, na mshinfi wa pili kumenyana na mshindi wa nne.
Simba SC ndio waliokuwa mabingwa msimu uliopita wakiifunga kwa penalti 3-1 dhidi ya watani, Yanga kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90, wakati Azam FC ilimaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gatew Uanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Simba ilifika Fainali kwa ushindi wa penalti pia 4-2 dhidi ya Singida Fountain Gate huku Yanga wakiifunga Azam FC 2-0.

0 comments:
Post a Comment