Friday, July 19, 2024

    ONANA NA AWESU WAWASILI KAMBINI ISMAILIA SIMBA SC


    VIUNGO washambuliaji, Awesu Ally Awesu (28) na Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana (24) wamewasili mjini Ismailia nchini Misri  kwenye kambi ya Simba SC kujiunga na wenzao kwa maandalizi ya msimu mpya.
    Sasa wachezaji wawili tu wanakosekana kwenye kambi ya Simba, beki Lameck Lawi aliyesajiliwa kutoka Coastal Union ya Tanga na kiungo mshambuliaji, Kibu Dennis Prosper.
    Kuhusu Lawi klabu yake imegoma kumruhusu na suala lao litaamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati Kibu imeripotiwa hajarejea kutoka Marekani alipokwenda kwa mapumziko.
    GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ONANA NA AWESU WAWASILI KAMBINI ISMAILIA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry